Kina Kirefu!!!!!!!! Mansu-li Mansoor Ally Mohamed a.k.a Mansu-Li, msanii wa hip hop na mwanaharakati wa kweli kutoka Africa Mashariki,Tanzan...

Kina Kirefu!!!!!!!!

Mansu-li

Mansoor Ally Mohamed a.k.a Mansu-Li, msanii wa hip hop na mwanaharakati wa kweli kutoka Africa Mashariki,Tanzania.
Mansoor alianza rasmi kujihusisha na HipHop miaka ya tisini,na baadhi ya wasanii waliompa ushawishi na kuanza kuandika kiswahili ni Saleh Jabir,Weusi Wagumu Asilia{W.W.A},Kwanza Unit{K.U},wakati huo akiwa shule ya msingi Mlimani,Dar es salaam sambamba na Kevin Mwaliosi na Adam Mzee,tulikuwa tuna kariri rap za kimarekani kama Guru,Mobb Deep,Nas na Snoopy!
Mansoor alianza rasmi kurekodi mwaka 2003 baada ya kufudhu kuingia fainali za rap chini ya Magic Fm Radio.
Wimbo wa kwanza uliitwa Poa tuu chini ya mtayarishaji Dj.Harmy B,ila haikufanya vizuri.
Mwaka 2006 mwezi wa 7 ,Mansoor alitoka na nyimbo inayoitwa Kina Kirefu chini ya Harmy B Production,huu ni wimbo ambao "ulinitambulisha rasmi kwenye game!!!"
Mwaka 2007 mwezi june,niliingia kwenye Kilimanjaro Muzik Awards kama msanii bora wa rap,ila sikubahatika kuchukua tuzo.
Kabla ya hapa mwezi march 2007 ,alifanya track inayoitwa Sina budi ,kiitikio kikifanywa na Joselyn chini ya mtayarishaji D-money.
Baada ya utoaji wa Tuzo za Kilimanjaro kumalizika ,mansoor ametoa pini nyingine inayoenda kwa jina la Sura ya mchezo ambapo kwa sasa unatamba na video inatayarishwa na Chapakazi Filmz ambao pia 2006 walifanya nae video ya Kina kirefu.
Panapo majaliwa Mansu-li atatoka na album yake ya kwanza mwishoni mwa mwaka huu!!!